BETI NASI UTAJIRIKE

MANCHESTER UNITED YAENDELEA KUTESEKA 2022

 Klabu ya Manchester United imeuanza mwaka 2022 kwa kipigo cha bao 1 dhidi ya Wolvehampton Wanders mchezo wa ligi kuu  uliopigwa dimba la Old Trafford.


 Kikosi cha Manchester united kinachonolewa na kocha Ralf Rangnick kilishindwa kuonyesha makali ya mchezo baada ya kutawaliwa dakika zote za mchezo huku kikipiga mashuti mawili tu yaliyolenga golini.

Joao Martinez ndiye aliyewapa uongozi Wolverhampton baada ya shuti lake kuzama golini dakika ya 82 ya mchezo huo uliotawaliwa na kadi 4 za  njano. 

Beki Phil Jones alirejea uwanjani kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje ya dimba kwa siku  708 akicheza nafasi ya ulinzi wa Kati na Rafael Varane huku Wan Bissaka na luke show wakicheza nafasi ya beki wa kulia na kushoto. Mc Tomminay na Matic wao walianza kama viungo wakabaji huku Sancho na Greenwood wakianza kama viungo washambulia lakini nafasi zao zilichukuliwa na Marcus Rashford na Bruno Fernandes huku Ronaldo na Cavani walioanza nafasi za washambuliaji chini ya mfumo wa 4-2-2-2.

Matokeo hayo yanawafanya Manchester United washuke mpaka nafasi ya 7 wakiwa na point 31 kwenye michezo 19 waliyocheza wakishinda michezo 9 sare 4 na kupoteza 6.

Post a Comment

0 Comments