BETI NASI UTAJIRIKE

LIONEL MESSI AUANZA MWAKA 2022 KWA MAJANGA

 Lionel Messi ni miongoni mwa wachezaji wanne wa Paris St-Germain waliopimwa na kukutwa na Covid-19.


Mshambuliaji huyo wa Argentina na wachezaji wenzake Juan Bernat, Nathan Bitumazala na Sergio Rico walithibitishwa kuwa na Covid siku moja kabla ya mechi ya PSG ya Kombe la Ufaransa dhidi ya Vannes ya daraja la nne.

Wachezaji hao wanasemekana kuwa wamejitenga..Bosi wa PSG, Mauricio Pochettino aliongeza kuwa Messi alibaki Argentina ambako alikuwa mapumziko ya majira ya baridi na hatasafiri hadi atakapopimwa tena na kukutwa hana virusi.

Wakati wa mkutano na wanahabari kabla ya mechi Jumapili, Pochettino alisema hawezi kusema tarehe ambayo Messi atarudi.

Mchezo wa kwanza wa ligi wa PSG 2022 baada ya mapumziko yao ya msimu wa baridi ni dhidi ya Lyon ni Jumapili, Januari 9.

Wakati Neymar atakosa mechi hiyo huku akiendelea kupata nafuu kutokana na jeraha la mguu nchini Brazil.

PSG wanasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anatarajiwa kurejea mazoezini baada ya wiki tatu.

Post a Comment

0 Comments