BETI NASI UTAJIRIKE

HATIMAYE STAA WA SIMBA APATA TIMU KENYA

 Aliyewahi kuwa mchezaji wa Gormahia na baadaye Simba SC Fransis Kahata amefanikiwa kupata timu nyingine nchini Kenya.Mchezaji huyo mwenye miaka 29 amefanikiwa kujiunga na timu ya Polisi Kenya akitokea Sidama Coffee .


HISTORIA YA FRANCIS KAHATA 

Kahata alianza Soka lake katika klabu ya Thika United Academy  mwaka 2005-2009 na baadaye 2010 alijiunga timu ya wakubwa kisha kutolewa kwa mkopo kwenda United Pretoria kuanzia July 1 2010 ambako alihudumu kwa miezi michache na kurejea Thika United    December 31  

Msimu wa 2013/14 Alijiunga na KF Tirana kwa mkopo na alirejea tena Thika United ambako msimu wa 2014/15  Alijiunga tena KF Tirana kama mchezaji huru.

Julai 1 mwaka 2015 Star huyo alijiunga rasmi Gor Mahia kwa ada ambayo haikuwekwa wazi na aliitumikia timu hiyo Sambamba na Meddie Kagere kuanzia msimu wa 2015 mpaka 2019 kisha aliuzwa kwenda Simba.

Nyota huyo alihudumu Simba msimu wa 2019 mpaka 2021 akiisaidia timu hiyo kutwaa makombe ya FA,Ligi kuu na timu hiyo kufanikiwa kuingia robo fainali kwenye michuano ya CAF Champions league.Julai 2021 Aliachana na Simba na kujiunga Sidama Coffee kuanzia september 2021 na sasa amenaswa na Police Kenya Football Club. 

Post a Comment

0 Comments