Mchezo wa ligi kuu Uingereza kati ya Liverpool dhidi ya Chelsea uliopigwa Stamford Bridge umeibua gumzo baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa mabao 2-2.
Liverpool walikuwa wa kwanza kupata mabao hayo yaliyofungwa na Sadio Mane dakika ya 9 huku bao la pili likiwekwa kimiani na Mohamed Salah dakika ya 26. Chelsea walirejea kwa kasi zaidi na dakika ya 42 walijipatia bao la kwanza kupitia Kovavic huku Pulisic akisawazisha dakika ya 45
mpaka mpira unamalizika Chelsea 2-Liverpool 2.Matokeo hayo yanaifanya Manchester City izidi kuongoza kwa tofauti ya pointi 10 baada ya kuwa na pointi 53 kwenye michezo 21 waliyocheza wakifuatiwa na Chelsea wenye pointi 43 na Liverpool wenye pointi 42 huku Arsenal akiwa na pointi 35 nafasi ya 4.
0 Comments