BETI NASI UTAJIRIKE

BILA TSH 29000 HUTAKIWI KUIZUNGUMZIA YANGA

 Mwakilishi wa GSM  ndani ya Klabu ya Yanga Eng.Hersi Said  ameagiza kuwa mashabiki wote wa klabu hiyo kuhakikisha wanatoa shiringi 29000 kama ada ya uanachama kabla hawajaizungumzia Yanga kwenye magroup ya Whatsapp.



Kauli hiyo ameitoa wakatio yanga ikiingia mkataba na kampuni za N-CARD na KILINET kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za utambuzi wa wanachama na mashabiki wa klabu hiyo. Hersi amenukuliwa akisema 

"Napenda kuwashukuru KILINET na NCARD kuwa hapa na leo tunakwenda kufanya jambo la historia kubwa, tuwashukuru pia waandishi wa habari na wanahabari waliohudhuria hafla hii.Leo baada ya kusaini hapa idara ya Hassan Bumbuli na Haji Manara inatakiwa ifanye kazi kwelikweliwale mashabiki wa Yanga twende kuiongezea thamani timu yetu kiuchumi,isiishie watu wanachat kwenye magroup ya Young Africans especially maadmin asichat mtu yeyote kwenye group la Yanga mpaka uhakikishe amelipia muamala wa mwanachama kwanzia sasa hivi na hiyo ndiyo policy yetu.Hatutaki watu ambao hawana mchango kwenye timu yetu,unataka kutoa mawazo yako tuonyeshe Identification kama wewe ni mwanayanga na muamala wa shilingi elfu 29,000.


Post a Comment

1 Comments