BETI NASI UTAJIRIKE

RAISI BARCELONA AFUNGUKA KUMSAJILI HALAAND

 Baada ya Real Madrid kuwekeza nguvu kubwa ili iweze kumnasa Kylian MBappe mwishoni mwa msimu huu ,wapinzani wao wa jadi Barcelona wao wamewekeza nguvu kwa Eerling HalaandHalaand anayekipiga Borrusia Dortmund amekuwa na kiwango kizuri tangu kujiunga na klabu hiyo ya Ujerumani huku pia akiwa na ndoto za kuchezea vilabu vikubwa duniani kama Real Madrid na Barcelona huwenda ndoto zake zikatimia miezi michache ijayo baada ya raisi wa Barcelona Joan Larpota kuweka wazi mpango wao wa kujenga timu yao wakitumia wachezaji wa umri mdogo.

Larpota alitoa maoni yake juu ya uhitaji wao wa Halaand wakati wakimtambulisha Ferran Torres mchezaji mpya aliyejiunga kwa dau la paundi milioni 45 akitokea Manchester City.Mwandishi wa habari alihoji mipango ya Barcelona kumnunua Halaand naye Larpota alinukuliwa akisema

 "Unaniruhusu kumzungumzia mchezaji moja kwa moja lakini haitatupa faida sisi zaidi itaongeza thamani ya mchezaji huyo. Tunapambana kujiimarisha lakini pia tunapambana kuimarisha safu ya wachezaji"

Barcelona italazimika kutoa kiasi cha Euro milioni 75 ili kuweza kumnasa mchezaji huyo wa Dortmund na taifa la Norway

Post a Comment

0 Comments