BETI NASI UTAJIRIKE

BARCELONA WAMTAMBULISHA MCHEZAJI MPYA

 Klabu ya Barcelona chini ya Xavi Henandez imeanza kujijenga upya kwa kununua wachezaji mbalimbali hususani wenye umri mdogo.leo hii Barcelona imefanya utambulisho rasmi wa kiungo Ferran Torres 


Torres mwenye miaka 21 amejiunga na miamba hiyo ya Hispania akitokea Manchester City kwa dau la paundi milion 45.Torres ni mchezaji anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na mara zote amekuwa akionyesha kiwango kizuri akicheza nafasi ya winga wa kulia 

Mchezaji huyo alianza safari yake ya kisoka katika klabu ya Valencia mwaka 2017 mpaka 2020 aliponunuliwa na matajiri wa Manchester ,Manchester City ambapo aliitumikia klabu hiyo mpaka kwa msimu wa 2020/21 na 2021/22 mwanzoni alipouzwa kwenda Barcelona.

Torres amekwisha itumikia u21 ya timu ya taifa ya hispania na 2020 aliitwa rasmi kuitumikia timu ya taifa hilo.Akiwa Manchester City alicheza michezo 28 na kufunga mabao 9 huku timu ya taifa Hispania akicheza michezo 20 na kufunga mabao 12

Post a Comment

0 Comments