Rekodi tatu zilizowekwa usiku wa ligi ya mabingwa ulaya (uefa)

 Ligi ya mabingwa ulaya iliendelea usiku wa jana hatua ya makundi kutoka kundi A mpaka kundi D raundi ya 6 huku tukishuhudia baadhi ya timu kuendelea na hatua ya 16 bora nyingine michuano ya Europa league huku timu zingine zikiondolewa jumla kwenye michuano hiyo.

Michezo hiyo iliweka rekodi mbalimbali kwa wachezaji na timu zao. Na hizi ni rekodi zilizotikisa michuano hiyo.

1.Sebastian Haller ameweka rekodi ya kuwa mfungaji wa pili kufunga kila mchezo wa hatua ya makundi baada ya kucheza michezo 6 na kufunga mabao 10 na rekodi hii inamfanya nyota huyo wa ajax kuwa sawa na Ronaldo aliyeweka rekodi hiyo mwaka 2017-18.Maabao hayo 10 aliyofunga yameiwezesha Ajax kufuzu hatua ya 16 wakiwa na point 18 na hii ni rekodi mpya kwa klabu hiyo yenye makazi yake nchini uholanzi

2.Eerling Halland ameendelea kuweka rekodi ndani ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya akicheza jumla ya michezo 19 na kufanikiwa kufunga  mabao 23 akiwa na miaka 21. Haaland alikuwa vyema tangu msimu wa 2020/21 baada ya kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kufunga mabao 10.

3.Messi amefanikiwa kuvunja rekodi ya Pele baada ya kufunga jumla ya mabao 768 na kumfanya awe mchezaji namba mbili mwenye mabao mengi nyuma ya Cristiano Ronaldo. Messi alifunga mabao mawili usiku wa jana dhini ya club brugge na kusaidia timu yake kuingia hatua ya mtoano

Post a Comment

0 Comments