YANGA HII HAISHIKIKI AISEE ,FEISAL AWA GUMZO

Klabu ya Yanga SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwalaza wenyeji, wahamiaji KMC mabao 2-0 jioni ya leo Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Nyota wa mchezo wa leo ni kiungo wa kimataifa nchini, Feisal   Salum Abdallah aliyefunga mabao yote mawili mapema kipindi cha kwanza na kuifanya timu ya kocha Mtunisia, Nasreddine Nabi anayesaidiwa kazi na Mrundi, Cedric Kaze ifikishe pointi tisa baada ya mechi tatu za awali, mbili ikicheza ugenini. 

Fei Toto, alifunga bao la kwanza dakika ya tano baada ya kufumua shuti kali lililombabatiza mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele kufuatia kudondoshewa mpira na kiungo mwingine, Mkongo Yannick Bangala aliyeuzuia mpira uliookolewa na mchezaji wa KMC.Mzanzibari huyo akafunga bao la pili dakika ya 12 kwa shuti kali pia la umbali wa mita mita 25 baada ya kutengewa pasi na Mayele.


Post a Comment

0 Comments