BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO IJUMAA TAREHE 22 /10/2021

 Real Madrid watamkosa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland,21, huku Manchester City, Paris St-Germain au Bayern Munich kuna uwezekano mkubwa akatua huko. (AS - in Spanish)

Manchester United na Chelsea zinamtaka pia mshambuliaji huyo Mnorway, ambaye anataka mshahara wa zaidi ya £30m kwa mwaka. (ESPN)

Borussia Dortmund wamekasirishwa na kitendo cha kocha wa Chelsea Thomas Tuchel kuzungumza hadharani kuhusu nia ya klabu yake ya kumsajili Haaland. (Bild, via Mirror)

Everton wanamtaka kiungo wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28, mwezi Januari. (Football Insider)

Barcelona inataka kuishinda Real Madrid katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa PSG na Ufaransa Kylian Mbappe, ambaye mkataba wake unamalizika msimu unaokuja. (AS - in Spanish)

Kiungo wa Manchester United Donny van de Beek, 24, hatarudi Ajax lakini kuna nafasi kubwa kwamba ataondoka Old Trafford. (Fabrizio Romano) 

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer anasema klabu hiyo haijapokea ofa kutoka Everton kwa ajili ya kiungo wake wa Uholanzi Van de Beek, licha ya uwepo wa tetesi nyingi. (RTL7, via Manchester Evening News)

Liverpool, Manchester United na PSG walimpa ofa ya pesa nyingi Ansu Fati ili ajiunge nazo kabla ya kinda huyo mwenye miaka 18 mzaliwa wa Guinea-Bissau, mchezaji wa kimataifa wa Hispania kusaini mkataba mpya Barcelona. (Cope)

Mlinzi wa Juventus Giorgio Chiellini anasema ingekuwa bora mshambuliaji wa Ureno wa Cristiano Ronaldo, 36, kuondoka Juve na kujiunga na Manchester United mapema zaidi. (DAZN, via Goal)

Kiungo wa zamami wa Arsenal na England Jack Wilshere, 29, yuko tayari kuhamia ligi kuu ya Marekani kujiunga na klabu ya Inter Miami. (Talksport)

messi

Arsenal imepinga taarifa kwamba imemsajili mtoto wa miaka 4 ambaye amepata umaarufu kupitia mtandao wa Instagram baada ya kuzagaa kwa video zake zikionyesha kipaji chake kikubwa na kusema 'Messi mtoto' huyo ni mmoja wa wachezaji watoto walioko kwenye vituo vyake. (Sun)

Post a Comment

0 Comments