BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA LEI ALHAMIS TAREHE 21 OKTOBA 2021

 Mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele, yuko tayari kuhamia Newcastle United wakati mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 24, alijiunga na klabu hiyo ya Catalan kwa ada ya £117m mwaka 2017. (Goal)


Jana Jumatano Newcastle imemfanyia usaili kocha wa zamani wa Roma Paulo Fonseca kupitia njia ya mtandao wa Zoom, mreno huyo mwenye umri wa miaka 48 anaonekana kuongoza katika makocha wanaowaniwa kumrithi Steve Bruce. (Daily Mail)

Wamiliki wapya wa Newcastle bado hawajafikia uamuzi wa mwisho kuhusu kocha wa kumuajiri, huku kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez, meneja wa zamani wa Chelsea Frank Lampard, kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Lucien Favre, kocha wa Rangers Steven Gerrard na kocha wa zamani wa Bournemouth Eddie Howe bado wanaendelea kufuatiliwa. (Guardian)

Chelsea wanamtaka mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21, kutoka Borussia Dortmund, anasema kocha wa timu hiyo Thomas Tuchel. (Bild via The Sun)Manchester City wanamsaka mshambuliaji wa Fiorentina, Mserbia Dusan Vlahovic, 21. (Tuttosport via Manchester Evening News)Vilabu vya Manchester City na mahasimu wao Manchester United vinafikiria kuchuana na Barcelona katika mbio za kusaka saini ya mshambuliaji wa RB Leipzig na Hispania Dani Olmo. (Christian Falk on Twitter)

Kiungo wa Leicester City Mbelgiji Youri Tielemans, 24, amekataa ofa ya kuongeza mkataba, na kuvifanya vilabu vya Manchester United, Chelsea, Liverpool, Real Madrid, Atletico Madrid na Bayern Munich kukaa mguu sawa. (90 mins)

Tottenham imejiunga katika orodha ndefu ya vilabu ikiwemo West Ham -ya ligi kuu England kumfuatilia mshambuliaji wa Genk Paul Onuachu. Klabu yake hiyo ya Ubelgiji inataka ada ya £20m ili kumuachia Mnigeria huyo ngongoti mwenye urefu wa zaidi ya futi 6ft(Daily Mail)

Brighton wanamfuatilia mshambuliaji wa Clermont raia wa Guinea, Mohamed Bayo, 23, ambaye klabu yake hiyo ya Ufaransa inataka ada ya £10m, Bayo amekuwa akifananaishwa na mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku. (Argus)

Kiungo mreno Bruno Fernandes, 27, alitishia kuondoka baada ya kusikia klabu yake ya Manchester United ilikua moja ya vilabu 12 vilivyosaini mpango wa kuanzishwa kwa ligi mpya ya Ulaya "European Super League. (The Athletic)

th

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27, anakaribia kabisa kusaini mkataba mpya na vigogo wa Italia Juventus, anasema makamu wa rais wa klabu hiyo Pavel Nedved. (Football Italia)

Sheffield United bado wanamuania kumsajili winga wa Barcelona, mhispania Alex Collado, 22 baada ya kushindikana kumsajili katika dirisha lililopita la majira ya joto. (Mundo Deportivo via Sport Witness)

Post a Comment

0 Comments