BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA YAWEKA REKODI MPYA TUZO ZA TFF (TFF AWARDS )

 Klabu ya Simba imeibuka kinara usiku wa leo kwenye tukio la utoaji wa tuzo za TFF baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo mbali mbali kuanzia mchezaji bora wa msimu,mfungaji bora wa msimu,beki bora ,kipa bora na kiungo bora wa Msimu.


Kapteni John Bocco ndiye aliyekuwa kinara wa tuzo hizo kwa kuondoka na tuzo tatu kubwa ikiwamo ya Mfungaji Bora,Mchezaji Bora wa Msimu na kuwemo kwenye listi ya kikosi bora cha msimu wa 2020/21

Mohammed husein ambaye ni kapteni msaidizi alitwaa tuzo ya beki bora huku akiingia katika kikosi bora cha msimu,Clatous Chama na yeye alitwaa tuzo ya kiungo bora wa msimu na kuingia kwenye kikosi cha wachezaji 11 .

Kocha wa Simba Didier Gomez Da Rosa ameibuka kocha bora wa msimu baada ya kuiwezesha timu hiyo kutwaa makombe ya ligi kuu pamoja na Azam Sports Football Cup.

Aishi Manula aliibuka kipa bora wa msimu kwa mara ya tano mfululizo baada na ameingia kwenye kikosi bora cha msimu na kumfanya aendelee kuwa nambari moja nchini.Shomari Kapombe na Luis Miquisone wameingia kwenye kikosi bora cha TFF kwa msimu wa 2020/21.

Hizi ni picha za wachezaji wa Simba wakitwaa tuzo hizo


Post a Comment

0 Comments