BETI NASI UTAJIRIKE

MZAMBIA KIBOKO YA HAALAND APIGA GOLI NNE EUROPA

 Patson Daka si jina geni kwa wafuatiliaji wa ligi kuu Uingereza ,mchezaji huyu wa Leicester amejizolea umaarufu msimu huu baada ya kufunga bao la nne dhidi ya Manchester united kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Oktoba 16,2021. Daka alitokea benchi dakika ya 77 na kufunga bao murua dakika ya 94

Kilichonifanya nimuandike mzambia huyu ni rekodi mbili kubwa alizoweka kwa msimu huu kwenye michuano ya EUROPA  baada ya kufunga mabao manne peke yake dhidi ya Spartak Moscow. na ile ya kuwa mzambia wa kwanza kuichezea Leicester City akitokea sub na kufunga bao dhidi ya Manchester United

HISTORIA KWA UFUPI

Daka alizaliwa 9 Oktoba 1998 huko Zambia na ni mchezaji anayechezea timu ya Taifa hilo, Daka alianza safari yake ya soka kwa kuchezea timu ya under 12 Kafue Celtic akatolewa kwa mkopo kwenda Nchanga Rangers na baadaye Power Dynamo zinazoshiriki ligi kuu Zambia.

2017 alihamia Austlia na kujiunga na RB Salzburg kama mchezaji wa akiba na 2018 aliingia kikosi cha kwanza na kuisaidia timu hiyo kutwaa makombe matatu ya ligi (AUSTRIAN BUNDESIGA) na makombe matatu ya ligi (AUSTRIAN CUP)

2021 Alijiunga na Leicester City na mpaka sasa amecheza michezo 3 ndani ya timu hiyo akifunga mabao 5 ,Daka anarekodi nzuri kwa upande wa ulaya baada ya kuisaidia RB Salzburg kufunga mabao 27 kwenye mechi 28 alizocheza kwa msimu wa 2020/21.

UKARIBU WAKE NA HAALAND 

Msimu wa 2019/20 Halaand alijiunga na RB Salzburg akitokea Molde na walishirikiana vyema na Daka .Mwisho wa msimu Halaand alimaliza mfungaji bora kwa kufunga mabao 17 kwenye michezo 16 aliyocheza huku Daka akifunga mabao 24 kwenye michezo 31 aliyocheza wallipa timu hiyo makombe mawili ya Bundesliga na Austrian CUP



Post a Comment

0 Comments