BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAFUNGA BARABARA ZOTE ZA TABORA

 


Klabu ya Yanga imefanikiwa kuwasili salama mkoani Tabora kwenye mchezo wa kombe la shirikisho Azam (Azam Sports Federation Cup)nusu fainali dhidi ya  Biashara United mchezo utakaopigwa ijumaa hii katika dimba la Ali Hassan Mwinyi .

Mchezo huu unategemewa kuwa kivutio kwa mashabiki wa soka nchini kwani mshindi atakwenda kucheza fainali moja kwa moja. Wachezaji na viongozi wa Yanga waliwasili Tabora kwa ndege ya Air Tanzania nawalipokelewa na mashabiki wa timu hiyo jambo lililosababisha foreni kubwa barabarani na njia zote za mjini kufungwa.

Hii ni video ikionyesha namna mashabiki hao walivyofunga barabara zote za mjini TaboraPost a Comment

0 Comments