BETI NASI UTAJIRIKE

AZAM WAIJIBU SIMBA MAJEMBE MANNE YAKIREJEA NYUMBANI SONGEA



Mashabiki wa klabu ya Azam huko Songea hawajakaa kimya na wameliamsha dude kuelekea mchezo wa kombe la shirikisho hatua ya nusu fainali mchezo utakaopigwa siku ya jumamosi ya tarehe 29 June mjini hapo.

Awali wachezaji wa Simba waliwasili mjini hapo kwa shirika la ndege Air Tanzania na kupokewa na mashabiki lukuki ndipo rundo la mashabiki wa Azam FC walipojitokeza jioni ya leo kupokea msafara na wachezaji wa timu hiyo uliowasili uwanjani hapo kwa shirika la ndege la Air Tanzania. 

Mapokezi hayo ya kishujaa yamewafanya Azam kutambua umuhimu wa mchezo huo na hiyo ni tafsiri tosha kwamba mchezo huo ni muhimu sana kwa mashabiki.Jambo zuri zaidi ni kurejea wachezaji wazawa wa songea  wa klabu hiyo akiwemo kipa Benedict Haule,Frank Domayo Agrey Morris na Abdallah Kher 

haya ni mapokezi waliyoyapata Azam FC 





Post a Comment

0 Comments