BETI NASI UTAJIRIKE

ZANA COULIBALY ALAMBA DILI JIPYA

Klabu ya soka ya Medeama inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ghana, imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa zamani wa klabu ya Simba raia wa Ivory Coast, Zana Coulibally ambaye amejiunga nao kwa mkataba wa miaka miwili.

Beki huyo amesajiliwa kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya AS Vita ya DR Congo mwishoni mwa msimu wa mwaka jana.
Taarifa rasmi ya Medeama imeeleza: "Medeama inayofuraha kutangaza kukamilisha usajili wa beki wa kulia raia wa Ivory Coast, Coulibaly Zana Oumar kwa mkataba wa miaka miwili, anajiunga na Mauve na Njano kutoka kwa wababe wa DR Congo klabu ya AS Vita.

“Coulibaly amewahi kupita katika klabu za Africa Sports, ASEC Mimosas, na timu yenye nguvu kutoka Tanzania Simba SC, ambapo akiwa na Simba nyota huyo mwenye miaka 27 alikuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19.”

Post a Comment

0 Comments