BETI NASI UTAJIRIKE

SABABU ZILIZOMFANYA LEWANDOWSKI AKAWAPOTEZA RONALDO NA MESSI

Mshambuliaji wa Bayern Munich ameibuka mchezaji bora kwa mwaka 2020 baada ya kuwamwaga Ronaldo na Messi kwenye tuzo hizo. Lewandowski anakuwa mchezaji wa tatu kuwawi kutwaa tuzo ya Fifa Pro baada ya Ronaldo kutwaa mara 2 na Lionel Messi akitwa mara 1.Binafsi naungana na FIFA kumpongeza mchezaji huyo kutokana na ubora wake aliouonyesha kwa msimu wa 2019/20 na ubora huo umeinufaisha klabu yake ya Bayern Mnich huku yeye mwenyewe akiweka rekodi mpya. Hizi ni sababu zilizopelekea Lewandowski kuwafunika Ronaldo na Messi.

1.Mabao
Kwa msimu wa 2019/20 Lewandowski amecheza michezo 47 akifunga mabao 55 na kutengeneza mengine 10. kwa takwimu hizo ni wazi ametengeneza mabao 65 kwenye mechi 47 tu alizocheza na kumfanya aonekane tishio. Mshambuliaji huyo alikuwa kinara wa mabao UEFA CHAMPIONS LEAGUE baada ya kufunga mabao 15 kwenye mechi 10 alizocheza huku pia akifunga mabao 34 kwenye mechi 31 za Bundesliga.

2. Mafanikio kwa timu
Lewandoski ameiwezesha Bayern Munich kutwaa makombe matatu makubwa waliyoshiriki ikiwamo Ligi ya Mabingwa Ulaya ,Bundesliga na DFB Pokal kwa uwezo huo ameonekana ni nyota tegemezi zaidi kwa mabingwa hao wa ulaya
 
3.Tuzo Mbali mbali 
Lewandowski alitwaa tuzo ya mchezaji bora na mfungaji bora wa Bundesliga huku pia akitwaa tuzo za mchezaji bora na mfungaji bora wa UEFA na sasa ametwaa tuzo za FIFAPRO kwa mwaka 2020

Post a Comment

0 Comments