BETI NASI UTAJIRIKE

ROONEY ASAJILIWA MANCHESTER UNITED

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney amefanikisha dili la mtoto wake Kai Wayne Rooney kujiunga na Manchester United. 

Kai mwenye umri wa miaka 11 atajiunga na Manchester United academy na kuna uwezekano akadumu klabuni hapo kwa miaka mingi

Kai alizaliwa mwaka 2009  kwenye familia ya Coleen na Wayne Rooney na Kai ndiye mkubwa kuliko wenzake watatu. itakumbukwa Wayne Rooney alijiunga na Manchester United mwaka 2004 mpaka mwaka 2017 huku akiisaidia timu hiyo kutwaa makombe mbalimbali yakiwemo ya ligi kuu 5 ,FA,Carling Cup na Champions Ligi 1 mwaka 2008. 

Rooney anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi ndani ya Manchester United akifunga mabao 254 bkwenye mechi 559 alizocheza.

Mara baada ya usajili kukamilika Wayne Rooney kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika |"Najiskia fahari kwa  Kai kusaini Manchester United, ongeza juhudi zaidi" naye Coleen aliandika "Usiku maalumu, hongera sana Kai,Nakupenda sana na najiskia fahari ,jitahidi uwezavyo

Post a Comment

0 Comments