BETI NASI UTAJIRIKE

MECHI 100 ZA RONALDO NDANI YA JUVENTUS

Cristiano Ronaldo ameendelea kuwa gumzo nchini  Italy baada ya kuweka rekodi ya kutimiza mechi 100 za kuitumikia Juventus. Nyota huyo alisajiliwa mwaka 2018 akitokea Real Madrid na ndiye mchezaji aliyenunuliwa kwa dau kubwa zaidi kwenye historia ya Serie A huku pia akiwa anaongoza kwa mshahara mkubwa kwenye ligi hiyo.Wiki iliyopita aliweka rekodi ya kufunga mabao 750 tangu aanze soka la kulipwa. Jumatano ya tarehe 9 disemba alifunga mabao mawili kwa mikwaju ya penati dhidi ya Barcelona kwenye ligi ya mabingwa ulaya. Leo jumapili akiwa kwenye mchezo wa Serie A amefunga mabao mawili ya penati na kumfanya afikishe mabao 10 kwenye michezo 7 aliyocheza mpaka sasa kwenye ligi hiyo.

Ronaldo amekuwa neema ndani ya Juventus kwani amefunga jumla ya mabao 79 akitengeneza mengine 19 na kumfanya awe na mchango wa mabao 98 kwenye mechi 100 alizokwisha cheza ndani ya juventus

Post a Comment

0 Comments