BETI NASI UTAJIRIKE

JESHI LA SVEN LIPO TAYARI KUIVAA FC PLATINUM

 Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo Ijumaa saa nne asubuhi wanatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza, utapigwa Disemba 23 huko ZimbabweKocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema ataondoka nchini na kikosi cha wachezaji 22 ambao watakuwa na jukumu la kuiwakilisha Simba na Tanzania kwa ujumla

"Tutaanza safari siku ya Ijumaa kwa ajili ya kuwafuata wapinzani wetu FC Platinum. Ninaamini tutakwenda kupambana na kufanya vizuri na msafara wetu utakuwa na jumla ya wachezaji 22"

"Hautakuwa mchezo mwepesi lakini tutakwenda kufanyanya vizuri, unajua kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huku ushindani wake ni wa tofaut"

"Kuhusu wachezaji ambao tutakwenda nao nitaweka wazi baadae kwani bado hatujafanya tathimini hasa baada ya kumaliza mchezo wetu dhidi ya KMC"

Mchezo wa kwanza ugenini unatarajiwa kuchezwa Desemba 23 na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Januari 6.

Post a Comment

0 Comments