BETI NASI UTAJIRIKE

HAPA KWA KOCHA BORA FIFAPRO WAMECHEMKA

Kocha wa Liverpool Jurgen Klop ameibuika kocha bora wa mwaka 2020 akiwamwaga Hans Flick wa Bayern Munich pamoja na Marcelo Bielsa wa Leeds United. Klopp ametwaa tuzo hiyo baada ya kutwaa ligi kuu uingereza kwa mara ya kwanza toka liverpool ilipofanya hivyo mwaka 1990.

Binafsi sikubaliani na maamuzi ya FIFA na naamini wadau wengine wataungana na mimi kwamba aliyestahiri tuzo hizi ni Hans Flick wa Bayern Munich. Chini ya Flick Bayern Munich msimu wa 2019/20  imefanikiwa kutwaa makombe matatu ikiwemo Bundesliga ,DFB Pokal na Uefa huku ikiwa imecheza michezo 57 ikishinda 49 ikipoteza michezo 3 na sare 5

Kwa mwaka 2020 Klopp amecheza michezo 55 akishinda 42 kupoteza 8 na sare huku akitwaa ubingwa wa ligi kuu Uingereza pekee. Swali ni kivipi Klopp akaibuka kocha bora wa mwaka ?maana kitakwimu ameachwa mbali kabisa na Flick. Hapa Fifa wametupoteza 

Post a Comment

0 Comments