BETI NASI UTAJIRIKE

BONDIA FRANK LUCIAN AWEKA REKODI NYINGINE

 Bondia Frank Lucian ameendeleza ubabe wake baada ya kumtandika kwa K.O bondia Ally Kombo Hamis kwenye pambano la uzito wa kati (Feather Weight.) mchezo uliopigwa ukumbi wa Dolphin jijini Dar es salaam tarehe 12 Disemba 2020.

Bondia huyo aliibuka na ushindi raundi ya 2  kwenye pambano lililokuwa na raundi 6 na kumfanya aweke rekodi ya kushinda mapambano 5 kati ya 6 aliyokwisha cheza. Bondia huyo ameshinda jumla ya K.O 4 ushindi wa pointi 1 na amepoteza 1 akiwa chini ya Bocca Boxing Club yenye makao yake makuu kimara jijini Dar es salaam chini ya Kocha Salum Lusasi.


Mara baada ya mchezo huo bondia huyo alinukuliwa akisema 
Nashukuru Mungu na mashabiki wangu pamoja na makocha wangu bila kuwasahau machampion wangu kwa kunipa sapoti. Namshukuru Mungu kwa ushindi wa K.O raundi ya pili naamini dua zenu zimefanya kazi na nawaahidi kuendeleza mapambano mpaka tufike juu zaidi. Kazi kazi chuma mlingoti chuma tuko pamoja 

Post a Comment

3 Comments