BETI NASI UTAJIRIKE

ZIFAHAMU TIMU TATU ZILIZOWAHI KUFUNGWA MABAO 8 UEFA


Klabu ya Barcelona imejikuta ikiandika historia chafu zaidi tangu kuanzishwa kwake na kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya baada ya kuruhusu kipigo cha mabao 8-2 dhidi ya Bayern Munich . Tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo tumeshuhudia vipigo vikubwa lakini kwa msimu wa 2019/20 Barcelona ndiyo timu ya kwanza kupokea kipigo kikubwa na kuifanya iingie kwenye orodha tmu zilizopigwa mabao mengi UEFA .

1.Liverpool vs Beskitas mabao 8-0

Mwaka 2007 ulikuwa ni mwaka wa moto kwa upande wa Liverpool .Kikosi hicho kiliibuka na ushindi wa mabao 8-0 pale pale Anfield na kuifanya timu hiyo kuogopeka zaidi ulaya .Yossi Benayoun alifunga mabao matatu kwenye mchezo huo huku peter crouch alifunga mabao mawili,Gerrard,Babel wakifunga bao moja kila mmoja . hiyo inabaki kumbukumbu kwa timu ya Liverpool.

2.Real Madrid vs Malmo mabao 8-0

Kwenye mchezo huu uliopigwa dimba la Bernabeu uliweka rekodi baada ya Cristiano Ronaldo kuweka rekodi ya kufunga mabao manne ndani ya dakika 19 huku Karim Benzema akifunga mabao matatu ndani ya dakika 79 uliwafanya vijana wa Kiswidishi wauchukie msimu wa 2015/16 msimu ambao Real Madrid walitwaa pia kombe la UEFA

3.Bayern Munich vs Barcelona 8-2

Bayern Munich bila huruma wameifanya Barcelona ionekane si kitu mbele ya uso wa dunia baada ya kuikandamiza mabao 8-2 mbele ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2019 Lionel Messi akiwa ndani. Mabao ya Muller Coutinho,mKimmich,Lewandowski,Gnabry na Perisic yameufanya msimu wa 2019/20 kuwa mbovu zaidi kwa Barcelona . Kipigo hicho kinaifanya Barcelona kuwa nafasi ya tatu kwa timu zilizofungwa mabao mengi zaidi UEFA.

Post a Comment

0 Comments