BETI NASI UTAJIRIKE

ZIDANE ASHINDWA KUIVUSHA REAL MADRID ROBO FAINALI


Klabu ya Real Madrid inayonolewa na Zinedine Zidane imejikuta ikikubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Manchester City kwenye mchezo wa 16 bora raundi ya pili mchezo uliopigwa dimba la ETIHAD jijini Manchester.

Raheem Sterling alikuwa wa kwanza kufungua nyavu za Real Madrid kwa kufunga bao murua dakika ya 9 ya mchezo huo huku Karim Benzema kisawazisha bao hilo dakika ya 28 ya mchezo.Gabriel Jesus ndiye aliyemaliza shuguli yote baada ya kufunga bao la pili kwa Machester City dakika ya 68.

Matokeo hayo yanaifanya Manchester City kuwa na mabao 4-2 dhidi ya Real Marid na moja kwa moja Manchester wanakwenda kucheza robo  fainali kwa msimu wa 2019/20

Post a Comment

0 Comments