BETI NASI UTAJIRIKE

BEKI MZEE ALIVYOWACHANYA MASHABIKI WA SIMBA


Beki Joash Onyango ametambulishwa rasmi ndani ya Simba. Beki huyo wa zamani wa Gor Mahia amewahi kucheza pamoja na Meddie Kagere pamoja na Francis Kahata alikuwa gumzo siku kadhaa baada ya picha zake akiwa na ndevu kusambaa mitandaoni na kumfanya aonekane mzee .

Sasa beki huyo ametua nchini na kutambulishwa rasmi na klabu ya Simba akiwa amenyoa ndevu zote hivyo kuonekana ni mchezaji kijana na kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo wasiamini kama ni mchezaji huyo waliyemuona kwenye picha za awali.

Ujio wa beki huyo mahili utazidi kuimalisha ngome ya ulinzi ya Simba kwani beki huyo ataungana na Ame,Nyoni,Wawa na Kennedy kwa eneo la ulinzi wa kati.Itakumbukwa msimu msimu uliomalizika Simba ndiyo timu pekee iliyoruhusu mabao machache.

Post a Comment

0 Comments