BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WATOA SABABU ZA KOCHA MKUU KUCHELEWA


Cedric Kaze raia wa Burundi ndiye anayetajwa kuwa kocha mpya wa Yanga akitokea kule Amerika ya Kusini ambako anafanya kazi.Bado wanayanga wanasubiri ujio wake, uongozi wa Yanga ukibainisha kuwa atawasili wiki hii tayari kuanza majukumu yake

Taarifa zaidi zimebainisha kuwa kilicho mchelewesha Kaze ni kusubiri majibu ya vipimo vya COVID-19 ili apatiwe vibali asafiri.Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema kocha huyo anaweza kuwasili kati ya kesho au Ijumaa

Lakini pamoja na kuchelewa, Kaze ameanza majukumu yake kwa ushirikiano na kocha msaidizi Riedoh Berdien ambapo inaelezwa ametuma program za mazoezi ya awali ambayo yanasimamiwa na Riedoh

Mwishoni mwa wiki hii Yanga inaweza kumtambulisha Kaze sambamba na wachezaji wengine waliosajliwa kwenye ufunguzi wa msimu wa wiki ya Mwananchi kule mkoani Dodoma siku ya Jumamosi August 22, 2020

Post a Comment

0 Comments