Kikosi cha Yanga kinaendelea na program za mazoezi kujiandaa na tamasha la Wiki ya Mwananchi pamoja na msimu mpya wa Ligi Kuu
Mapema leo, Bodi ya Ligi iliweka hadharani ratiba ya Ligi Kuu ambapo Yanga itaanzia nyumbani kwa kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo ambao utapigwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 06 saa moja siku
Leo beki wa kulia Kibwana Shomari aliyesajiliwa kutoka klabu ya Mtibwa Sugar aliripoti kambini na kujumuika katika mazoezi na wenzake walioanza mazoezi tangu wiki iliyopita
Mazoezi ya Yanga yanasimamiwa kikamilifu na kocha msaidizi mtaalam wa viungo, Riedoh Berdien
0 Comments