BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA MPYA NA YA KISASA INAKUJA


Mashabiki wa klabu ya Yanga wamejawa na furaha baada ya aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa Simba bw.Senzo Mbatha kutangaza kujiuzulu kisha kuhamia klabu hiyo yenye makao yake makuu Jangwani jijini Dar es salaam

Ni kama Yanga wanalipa kisasi kwa Simba baada ya klabu hiyo kumsajili Benard Morrison. Yanga kwa udhamini wa GSM wameendelea kufanya mabadiliko mbalimbali ndani na nje ya uwanja ikiwemo kufanya mabadiliko ya kimfumo,kujenga timu mpya na kutengeneza namna pekee kwa klabu hiyo kujiongezea kipato.

Uwepo wa Senzo ndani ya Yanga utaendeleza mafanikio ya klabu hiyo kwa msimu wa 2020/21 ikizingatiwa timu hiyo itacheza michuano ya kimataifa lakini kubwa zaidi ni kujenga timu imara kwa michuano yote

Senzo anakuwa ni mmoja wa wasaidizi wa Mwenyekiti Msolla lakini pia ataungana na timu ya La Liga inayoshughulikia mabadiliko ndani ya klabu hiyoPost a Comment

0 Comments