BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA KUSHUSHA KIFAA KIPYA KUTOKA HISPANIA


Taarifa isiyo rasmi ni kuwa klabu Yanga inajiandaa kumnasa aliyekuwa kiungo wa CD Tenerife Mtanzania Farid Mussa .Farid aliwahi kuichezea Azam FC na baadaye alipata dili kusajiliwa na timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Hispania.

Kwa sasa farid ni mchezaji huru na anahitaji changamoto mpya. Kwa tetesi tulizozipata ni kuwa Farid amekwishaanza  mazugumzo na Yanga na muda wowote anaweza kupewa mkataba na mabingwa hao wa kihstoria nchini.

Farid Mussa alinukuliwa akisema "Ni kweli nimekuwa nikitajwa kujiunga na klabu nyingi hapa Bongo hilo lipo wazi hasa kwa nyakati hizi za usajili.
"Ukweli ni kwamba kwa sasa mimi ni mchezaji huru na sehemu ambayo nitakuwa itajulikana hivi karibuni kwani uwezo huwa haujifichi na itakuwa wazi,".

Post a Comment

0 Comments