BETI NASI UTAJIRIKE

WAZIRI MWAKYEMBE ATOA MAAMUZI USAJILI WACHEZAJI WA KIGENI


Waziri Harrison Mwakyembe hii leo jumatatu Agosti 10 ametangaza rasmi uamuzi wa Serikali kuendelea kuruhusu idadi ya wachezaji 10 wakigeni. Kadhalika idadi ya wachezaji wanaotakiwa kuanza kucheza itabaki chini ya Baraza la Michezo BMT .Akitangaza uamuzi huo leo Dkt Mwakyembe amesema Serikali imezingatia maoni ya wadau .

Pia amesema bado wizara kwa kushirikiana na BMT na wadau wa soka watakaa kujadili aina ama viwango vya wachezaji wanaopaswa kusajiliwa na kuingia nchini.

"Angalau nchi zilizopo katika nafasi ya 50 kwa FIFA ndiyo tusajili huko hata wa daraja la kwanza, ingawa bado hii si sheria ni maoni tu"

"Ni vyema pia aina ya wachezaji watakaosajiliwa kutoka nje wawe na weledi, wawe na uwezo mkubwa"

Amesema kati watu 977 waliyotoa maoni ,watu 809 wametaka idadi ya wachezaji 10 wakigeni. Kando na hayo Wizara imeagiza watu wanaoajiriwa nchini wawe na ulazima wa kujifunza/kufunzwa Kiswahili..

Post a Comment

0 Comments