BETI NASI UTAJIRIKE

WADAU WAZUNGUMZIA JEZI NA LOGO MPYA YA SIMBA


Unapozungumzia mabadiliko ndani ya timu ni lazima utizame kuanzia ndani na nje ya timu. Kwa upande wa ndani uongozi wa Simba unaonekana kuleta mambo mazuri kuanzia wachezaji, kuondoa migogoro na hata namna ya kujiendesha .Kwa muonekano wa nje tunashuhusia uzinduzi wa viwanja vya mazoezi,ubebaji makombe na hata jezi za timu. Kwa hili mashabiki wa timu hiyo wamejikuta wakitembea vifua wazi kila mahali

Mashabiki wa klabu ya Simba wamefurahishwa na utambulishi wa jezi mpya na logo mpya ya timu hiyo kuelekea msimu wa 2020/21. Mashabiki hao wameonekana kufurahishwa na jezi hizo za aina tatu ambazo siku chache zijazo zitasambaa mitaani

Mashabiki hao wameungana na uongozi wa klabu hiyo kwenye utambulishi wa logo mpya wakisema logo hiyo imekaa kimataifa zaidi kama ilivyo klabu yao. Mashabiki hao wamesema kama Bayern Munich,Juventus ,Manchester City na hata Chelsea zilibadili logo wao ni akina nani mpaka wapinge mabadiliko.

Wewe kama mdau wa Amospoti unazungumziaje ujio wa jezi hizi mpya kwa msimu wa 2020/21 na vipi kuhusu hiyo logo

Post a Comment

0 Comments