TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU TAREHE 24-08-2020


Aston Villa itatangaza dau £30m la kumnunua mshambuliaji wa Celtic Mfaransa Odsonne Edouard, 22. (The Scottish Sun)
Kiungo wa safu ya kati-nyuma wa Lille raia wa Brazil Gabriel Magalhaes, 22, amekubali kujiunga na Arsenal na atakamilisha uhamisho wake wa £27m wiki ijayo. (The Guardian)
Bournemouth haitawazuia wachezaji wanaotaka kuhama - hatua ambayo imeifungulia mlango Manchester United kumsajili winga wa Wales David Brooks, 23. (Daily Mail)
Mkufunzi mpya wa Barcelona Ronald Koeman
Mkufunzi mpya wa Barcelona Ronald Koeman anataka kuwasajili mshambuliaji wa Inter Milan Muargentina Lautaro Martinez, 23, mlinzi wa safu ya kati na nyuma wa Manchester City Mhispania Eric Garcia, 19, na beki wa Valencia Mhispania Jose Gaya, 19. (Sport - in Spanish)
Klabu hiyo ya Catalan pia inamtaka kiungo wa safu ya kati ya nyuma wa Ajax Muargentina Nicolas Tagliafico, 27. (Marca)
Koeman pia angelipendelea mchezaji nyota wa Brazil Philippe Coutinho kuwa sehemu ya mpango wake - kiungo huyo aliye na umri wa miaka 28 amekuwa Bayern Munich kwa mkopo msimu huu. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Phillipe Coutinho alipochukuliwa na Bayern Munich kwa mkopo kutoka Barcelona
Newcastle wametoa ofa ya £4.5m kwa klabu ya Ugiriki ya PAOK kumnunua mchezaji wa safu ya kushoto - kulia Mgiriki Dimitris Giannoulis,24. (Manu Lonjon via Sports Lens)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anapania kumvuta kocha wa Brentford na mtaalamu Andreas Georgson kuwa sehemu ya kikosi cha ufundi. (London Standard)
Mshambuliaji wa klabu ya Tromso raia wa Norway Isak Hansen-Aaroen, 16, amethibitisha katika mitandao ya kijamii kuwa atahamia Manchester United. (Mirror)
Mike Arteta
Luis Figo hatarajii mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, akifuata nyayo zake kwa kuondoka Barcelona na kuhamia Real Madrid. (Marca)
Mshambuliaji wa Uswidi Zlatan Ibrahimovic, 38, bado hajasaini mkataba mpya AC Milan. Mchezaji nguli huyo atasalia bila timu mkataba wake utakapo kamilika mwisho wa mwezi Agost. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Mshambuliahi wa Juventus Cristiano Ronaldo "alimpendekeza" kiungo wa kati raia wa Portugal Bruno Fernandes, 25, kwa Manchester United, kulingana na beki wa zamani wa United Patrice Evra. (The Guardian)

Post a Comment

0 Comments