BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMANNE TAREHE 04-08-2020

Winga wa Chelsea Willian, 31, amekataa mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo na amekuwa akifanya mazungumzo ya uhamisho wa bure kwenda Arsenal, ambayo iko tayari kutoa mkataba wa miaka mitatu kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil kama anavyotaka mwenyewe. (Guardian)
Arsenal pia iko makini kumfuatilia mchezaji wa Bayern Munich raia wa Brazil Philippe Coutinho, 28, na kiungo wa kati wa Atletico Madrid raia wa Ghana Thomas Partey, 27. (Times - subscription required)
Mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang anataka kuona klabu hiyo ikimsajili mshambuliaji wa Barcelona mfaransa Ousmane Dembele, 23. (Le10 Sport)
Jadon Sancho
Maelezo ya picha,
Manchester United inakaribia kumsajili winga wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho katika mkataba wa karibia miaka mitano. (Mail)
Manchester United itahitajika kusubiri hadi kipindi cha mwisho kabisa cha usajili kumtafuta kiungo wa kati wa Uingereza Jack Grealish, 24 wa Aston Villa. (Mail)
England Ben Chilwell anashawishiwa na kujiunga na Chelsea
Maelezo ya picha,
Kocha wa Chelsea Frank Lampard ameshabaini walinzi watano tayari kuwauza na atafanya mikakati ya kumsajili Ben Chilwell, 23, beki wa kushoto wa Leicester City na Uingereza. (Times - subscription required)
Chelsea itahitajika kumfanya Chilwell winga wa thamani ya juu zaidi iwapo wanataka kumsajili. (Mirror)
Aidha, Chelsea inamnyatia beki wa kushoto wa Real Madrid na Uhispania Sergio Reguilon 23, ambaye amekuwa akitakiwa na Everton kwa uhamisho wa dau la paundi milioni 18. (Sky Sports)
Idrissa Gueye
Maelezo ya picha,
Paris St-Germain inataka kumuuza aliyekuwa kiungo wa kati wa Everton Idrissa Gueye na Wolves pia nayo inamnyapia mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal. (Le10 Sport)
AC Milan itakumbana na ushindani mkali kutoka kwa Bayer Leverkusen kwa mchezaji wa Norwich City anayesemekana kwamba thamani yake ni pauni milioni 30 mlinzi Ben Godfrey, 22. (Sky Sports)
Lazio, Tottenham, RB Leipzig, Everton na PSV Eindhoven zote zinamfuatilia beki wa kati wa Korea Kusini Kim Min-jae, 23. (Gazzetta dello Sport)
Danny Rose
Maelezo ya picha,
Mlinzi wa Tottenham na Uingereza Danny Rose, 30, anasema ni mwenye furaha mno kusalia kwenye klabu hiyo wakati anaingia msimu wa mwisho wa mkataba wake. (Second Captains Podcast, via Guardian)
Aston Villa, Leeds United, Newcastle United na West Ham zinania ya kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace na Jamuhuri ya Ireland James McCarthy, 29. (90Min)
Borussia Dortmund inakaribia kumsajili winga wa Manchester City, 15, Jamie Bynoe-Gittens. (Mail)

Post a Comment

0 Comments