BETI NASI UTAJIRIKE

SVEN AMESTAHILI KUWA KOCHA BORA ,MASHABIKI ACHENI MANENO


Mashabiki wa timu mbalimbali wamekosoa tuzo ya kocha bora aliyotwaa kocha wa Simba msimu wa 2019/20.Mashabiki hao wamesema kocha wa Namungo FC Thiery Hitimana alistahili kutwaa tuzo hiyo kwani aliipandisha ligi kuu timu ya Namungo FC huku msimu huu akiiwezesha kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Itakumbukwa kocha Sven alirithi mikoba ya Aussems aliyeondolewa na SIMBA mwanzoni kabisa mwa msimu wakiwa wamecheza michezo 7 . Sven aliiongoza timu hiyo vyema tangu alipokabidhiwa akiiwezesha timu hiyo kutwaa vikombe viwili msimu huu kile cha ligi kuu na FA.

Baadhi ya watu wamesahau kwamba Sven alishatwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi akifanya hivyo mara nne kwa msimu wa 2019/20. Kocha huyo asiyekuwa muongeaji sana amekuwa akiifanya Simba kucheza mpira wa kiwango cha uwezo wa juu sana na jambo la kushangaza ni kitendo cha kutompanga mara kwa mara mshambuliaji namba moja wa timu hiyo Meddie Kagere.

Sven huyu huyu ametengeneza kombinesheni hatari ya Chama ,Mkude,Fraga ,Miquissone, Kahata na Bocco kwa kipindi kifupi na kuifanya klabu ya Simba kuwa tishio kwa wapinzani wake.

Sven aliiongoza Simba kwenye michezo mbalimbali ukiwemo ule wa Singida United Simba wlipoibuka na ushindi wa mabao 8-0,Akiitoa Yanga hatua ya nusu fainali Asfc kwa kipigo cha mabao 4-1

Post a Comment

0 Comments