BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA WATANGAZA BALAA ZITO SIMBA DAY 2020


Klabu ya Simba imetangaza kufanya kufuru siku ya Simba Day itakayokuwa tarehe 22 Agosti 2020. Kupitia afisa habari wa klabu hiyo Haji Manara amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwani kutakuwa na mambo makubwa sana.

Manara amesema siku hiyo watalazimika kucheza na Vital O ya Burundi baada ya kushindwa kuileta Al Ahly kutokana na janga la Corona. Manara amenukuliwa akisema 


"Tulipanga kucheza na Al Ahly lakini changamoto ya corona imefanya jambo hilo kuwa gumu. Tunaamini Vital'O itatupa changamoto nzuri kwenye mchezo huo."
Vital'O itafika ijumaa saa 5 asubuhi na jioni timu zote zitafanya mazoezi kwenye uwanja wa Mkapa
Manara aliendelea kwa kusema Simba Day burudani itatolewa na Twanga Pepeta, Tunda Man, Meja Kunta, Mwasiti na kipekee atakuwepo Diamond Platinumz. Litakuwa kama tamasha la mziki, amekusudia kufanya jambo kubwa na kwa kupitia hilo kesho alhamisi kutakuwa na BIG SURPRISE kwa Wanasimba. MC atakuwa Mpoki

Uwanja wa Uhuru kiingilio kitakuwa ni Tsh. 2,000, kutakuwa na big screen na wachezaji na benchi la ufundi wakifika wataenda kwanza kule kusalimia."Watu 10 wa kwanza kukata tiketi za PLATINUM watapata nafasi ya kushiriki kwenye hafla ambayo itafanyika jumapili saa 1:00 usiku kwenye hoteli ya Serena ambayo wachezaji na benchi la ufundi watashiriki"

Post a Comment

0 Comments