BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA KUTUMIA SIMBA DAY KUTAMBULISHA NYOTA WAKE WAPYA


Klabu ya Simba SC imetangaza kwamba klabu ya VitalO ya Burundi ndiyo mgeni mwalikwa wa Simba day na  ndiyo klabu itakayocheza mchezo wa kirafiki siku ya Jumamos Agosti 22 mchezo utakaopigwa dimba la Benjamini  mkapa jijini Dar es Salaam.

Klabu ya Simba husherehekea Simba Day kila tarehe 8 August lakini kwa mwaka huu zoezi lilishindikana kutokana na mabadiliko ya ratiba ya ligi kuu kuchelewa kumalizika kutokana na janga la corona.

Simba wamefanikiwa kutwaa mataji matatu kwa msimu wa 2019/20 na sherehe hizo zinategemewa kupambwa na makombe hayo huku pia mechi hiyo ikitumika kuwatambulisha nyota kadhaa waliosajiliwa msimu huu akiwemo wakili msomi Benard Morrison ,Ibrahim Ame ,Onyango,Bwalya na wengine .

Post a Comment

0 Comments