ads

adds

SABABU ZA SENZO KUONDOKA SIMBA ZAWEKWA WAZI


Mkurugenzi mtendaji wa Simba Senzo Mbatha ametangaza kuachana na klabu ya Simba.Kupitia kurasa yake ya Twitter Senzo ameandika 

"Shukrani za kipekee kwa uongozi wa klabu ya Simba kwa kunipa nafasi ya kuiongoza klabu hii, Kwa masikitiko makubwa ninatangaza kuacha nafasi ya uongozi katika klabu. Ndani ya kipindi kifupi tumefanikisha mengi"

Chini ya uongozi wa Senzo klabu ya Simba ilifanikiwa kuwanasa nyota kadhaa akiwemo Miquissone pamoja na kocha Sven huku timu hiyo ikitwaa makombe matatu msimu huu.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema Senzo amekuwa akiingiliwa majukumu yake mbalimbali na baadhi ya viongozi wa klabu. Mmoja wa watu wa karibu na timu hiyo alisema 

"Unajua hapa klabuni bado kuna uswahili ,mfano Senzo hakutaka kabisa morrison asajiliwe kwa sababu anamfahamu kuwa ni mtovu wa nidhamu na ataleta usumbufu huko mbele lakini viongozi wengine wakamua kumsajili bila kumshirikisha hivyo jamaa ni kama amevunjiwa heshima kwenye nafasi waliyompa kwani masuala ya wachezaji yote ya wachezaji yanasimamiwa na CEO yeye anapeleka ngazi za juu kama una shauri lolote"

Mdau mwingine ndani ya Simba amenukuliwa akisema "Senzo amekuwa akilipwa mshahara mkubwa sana ndani ya klabu na alihitaji nyongeza zaidi nadhani uongozi ulimgomea au amekwisha pata timu nyigine . Simba ilifika mbali kabla ya ujio wake na hata akiondoka itafika mbali zaidi

Post a Comment

0 Comments