BETI NASI UTAJIRIKE

PSG YAPITA KIBABE NUSU FAINALI UEFA


Klabu ya Paris Saint German (PSG) imefanikiwa kutinga nusu fainali za michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa Msimu wa 2019/20. PSG iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Atlanta inayoshiriki Serie A italy.

Kwenye mchezo huo Atlanta walianza kwa kasi na dakika 26 ya mchezo walifanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia Mario Pasalic . Bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 90 kabla Marquinhos kuisawazishia PSG na Moting kufunga bao la ushindi dakika ya 90+3.

Matokeo hayo yanaifanya PSG kuwa timu ya kwanza kuingia fainali huku mchezo unaofuata hii leo ni RB.Leipzig dhidi ya Atletico madrid mchezo utakaopigwa saa nne usiku.

Kikosi cha PSG kilichoanza leo ni:Navas,Kehler,Silva,Kimpembe,Bernat,Herrera,Marquinhos,Gueye,IcardiNeymar,naSarabia

Post a Comment

0 Comments