BETI NASI UTAJIRIKE

OLYMPIC LYON KWISHA HABARI YAO SASA NI BAYERN VS PSG


Klabu ya Bayern Munich imefanikiwa kutinga fainali ya ligi ya mabingwa ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Olympic Lyon. Shukran za kipekee zimwendee Gnabry aliyefunga mabao mawili dakika ya 18 na 33 huku Lewandowski akifunga bao la tatu dakika ya 88 na bao hilo kumfanya afikishe mabao 15 kwenye michezo 10 aliyocheza.

Ushindi huo unaifanya Bayern Munich kucheza fainali na Paris Sain Germain waliofuzu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya RB Leipzig.Fainali ya michuano hiyo itapigwa tarehe 23 Agosti  kwenye dimba la Ataturk Olympic Stadium  lililopo jijini Istanbul Uturuki

Macho na maskio ya mashabiki wa soka yatahamia Uturuki kumshuhudia bingwa mpya wa michuani ya Ulaya kwani timu zote zimeonyesha uwezo mkubwa msimu wa 2019-20 mpaka kufika fainali.

Post a Comment

0 Comments