BETI NASI UTAJIRIKE

NYOTA WA AZAM YUKO NJIANI KUTUA JANGWANI


Kiungo mshambuliaji wa klbu ya Azam FC Abubakar Salum "Sure Boy" anapigiwa hesabu na klabu ya yanga kwa msimu wa 2019/20. Bado taarifa kamili hazijawekwa hadharani lakini viongozi wa Yanga wanaonekana kumwinda mchezaji huyo.

Yanga wamemsajili beki Bakari Mwamnyeto aliyekuwa akikipiga Coastal Union, Zawadi Mauya aliyekuwa anakipiga Kagera Sugar na Yasin Mustapha aliyekuwa anakipiga ndani ya Polisi Tanzania.

Usajili wa Sureboy ni mwendelezo wa kukijenga upya kikosi cha timu hiyo kitakachoshiriki michuano ya kimataifa msimu wa 20200/21 na hapo jana kilitangaza kuachana na nyota wake makini kama Ngassa,Molinga Tshishimbi na wengine 17

Chanzo cha kuaminika kimenukuliwa kikisema "Sure Boy yupo kwenye hesabu za Yanga na muda wowote anaweza kutambulishwa hivyo ni suala la kusubiri wakati," ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa Yanga ipo kwenye mchakato wa kuboresha kikosi hicho hivyo watafanya usajili makini.

"Tupo makini katika masuala ya usajili hatukurupuki ila wakati ukifika lazima tutaachia mchezaji mwingine," amesema.

Post a Comment

0 Comments