BETI NASI UTAJIRIKE

NIYONZIMA ATOA NENO KUHUSU USAJILI MPYA


Kiungo fundi wa Yanga Haruna Niyonzima ameeleza kufurahishwa na usajili unaofanywa na mabingwa hao wa kihistoria akiamini unakwenda kumaliza changamoto walizokuwa nazo msimu uliopita.Niyonzima amesema amefuatilia usajili huo kwa makini na amejiridhisha kuwa umezingatia kumaliza mapungufu yaliyokuwepo kiufundi

"Nafurahishwa na usajili unaoendelea ndani ya timu yangu . Ni usajili unaozingatia mapungufu yetu kimbinu na kiufundi pia kuipa timu nguvu ya kupambana kwa maana ya kutazama aina ya wapinzani wetu na malengo yetu kwa msimu wa 2020-21.
"Ubora wa klabu ni matokeo chanya na si vinginevyo nina imani ndicho ambacho viongozi wetu wamekilenga kwa sasa," amesema Niyonzima

Mnyarwanda huyo ni miongoni mwa wachezaji watatu wa kigeni waliobaki kwenye kikosi cha Yanga baada ya panga kali kupitishwa.Wengine ni mlinda lango Farouk Shikhalo na beki kisiki Lamine Moro

Yanga pia imekamilisha usajili wa nyota wengine watatu wakigeni ambao ni Yacouba Soghne, Tuisila Kinda na Mukoko Tonembe.Wachezaji wazawa waliotua Yanga ni Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Abdallah Shaibu, Bakari Nondo Mwamnyeto, Zawadi Mauya, Farid Mussa na Waziri Junior mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji wapya 10

Post a Comment

0 Comments