BETI NASI UTAJIRIKE

NIYONZIMA AIKACHA YANGA ATUA AZAM FC KIMYA KIMYA


Kiungo mchezeshaji raia wa Rwanda Ally Niyonzima amefanikiwa kuingia mkataba wa kuitumikia Azam FC kwa msimu wa 2021. Klabu ya Azam ilimtambulisha rasmi nyota huyo aliyekuwa anakipiga Rayon Sports ya nchini Rwanda.

Niyonzima alikuwa akiwindwa na klabu ya Yanga tangu msimu uliopita na alikwisha tengewa donge nono lakini dili hilo lilikwama kutokana na janga la Corona. Azam FC wamekuwa wakifanya usajili muhimu kuelekea msimu 2020/21 .

Uongozi wa Azam FC umesema mchezaji huyo anamkataba na klabu hiyo mpaka mwaka 2023 na pendekezo la kumsajili lilitoka kwa kocha mkuu Aristica Cioaba. Niyonzima anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na klabu hiyo msimu huu baada ya Awesu Awesu kutambulishwa siku ya Ijumaa. 

Picha ya Mkurugenzi mtendaji wa Azam Abdul Karim "Popat" akiwa na Ally Niyonzima 
Post a Comment

0 Comments