BETI NASI UTAJIRIKE

NGASSA NA YONDANI WAGEUKA DILI KWA TIMU YA MWANZA


Taarifa zinazosambaa kwa sasa ni kuhusu waliokuwa wachezaji wa Yanga Mrisho Ngassa na Kelvin kuhusishwa kuhamia timu iliyopanda daraja msimu huu Gwambina FCWachezaji hawa wote wawili walikuwa wanaichezea Yanga kwa msimu wa 2019/20 kabla ya kuchujwa na kutemwa na timu hiyo.


Ngassa mkataba wake uliisha ndani ya Yanga uongozi ulikataa  kumpa mkataba mwingine kisha Yondani ambaye naye mkataba wake uliisha na walikuwa kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba lakini waliposhindwana naye akapewa mkono wa kwa kheri.

Habari zinaeleza kuwa Gwambina ambayo msimu wa 2020/21 itashiriki Ligi Kuu Bara baada ya kupanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza imeanza kujiimarisha ili kuleta ushindani.
Habari kutoka ndani ya Gwambina FC zimeeleza kuwa tayari mchakato wa usajili umeanza huku majina ya wakongwe yakitajwa kusajiliwa.

"Kuna wakongwe ambao wanatazamwa ili kusajiliwa ndani ya Gwambina ikiwa ni pamoja na wale ambao wapo huru kama Yondani na Ngassa, hawa wanaweza kuongeza makali ndani ya kikosi," ilieleza taarifa hiyo,

Katibu Mkuu wa Gwambina FC, Daniel Kirahi amesema kuwa wamepanga kusajili wachezaji nane pekee huku akigoma kuzungumzia ishu ya Yondani na Ngassa.

Post a Comment

0 Comments