BETI NASI UTAJIRIKE

NEYMAR ATANGAZA VITA KUELEKEA MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA


Mshambuliaji wa PSG na Brazil Neymar Jr anaamini msimu wa 2019/20  ni zamu ya klabu hiyo kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza. Neymar ametimiza miaka mitatu tangu ajiunge na mabingwahao wa Ligue 1. 

Ikumbukwe Neymar alisajiliwa kwa dau la dollar milioni 263 na kumfanya awe mchezaji ghali zaidi duniani mpaka siku hii ya leo.Mchezaji huyo anamkataba wa miaka mitano na PSG wenye thamani ya dola milioni 350 mpaka mwaka 2022.

Neymar amekuwa na msimu mzuri baada ya kuiwezesha PSG kutwaa mataji manne kwa msimu wa 2019/20 huku wakiwa robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya na anaamini watatwaa kombe hilo.

Neymar alinukuliwa akisema "Nimejifunza mambo mengi sana ndni ya PSG kwa miaka hii mitatu,kuna nyakati za furaha lakini pia nyakati za huzuni hasa pale napokuwa nimekumbwa na majeraha.Shukrani kwa wachezaji wangu ambao wamekuwa wakinisapoti ninapokwama na ushirikiano wetu umetufanya tutwae makombe hayo manne.

inaishi maisha mazuri kwa sababu ya ushirikiano wa wachezaji na mashabiki wetu. Kwa msimu huu sisi kama familia engo letu ni kuacha alama kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na tunaamini tutatwaa kombe hilo.

Post a Comment

0 Comments