BETI NASI UTAJIRIKE

NAMUNGO WAZIDI JIIMARISHA WASHUSHA KIFAA KUTOKA AZAM FC


Idd Kipagwile anayekipiga nafasi ya Winga ametambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha  Namungo FC inayonolewa na Kocha Mrundi  Hitimana Thiery.

Kipagwile amesaini dili la mwaka mmoja ndani ya Namungo FC kwa mkopo akitokea Klabu ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Arstica Cioaba.Namungo FC ni miongoni mwa klabu ambazo zitapeperusha bendera ya Tanzania kwenye michuano ya kimataifa baada ya kuwa washindi wa nafasi ya pili kwenye Kombe la Shirikisho.

Nafasi hiyo wanaipata baada ya kucheza fainali na Simba ambayo ina taji la Ligi Kuu Bara hivyo Simba itawakilisha nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Namungo ikiwa kwenye Kombe la Shirikisho.

Post a Comment

0 Comments