BETI NASI UTAJIRIKE

JUMA ABDUL AFUNGUKA KILICHOMFANYA AACHANE NA YANGA


Aliyekuwa nahodha msaidizi wa klabu ya Yanga Juma Abdul mnyamani amemwagana na klabu ya Yanga.Taarifa zinasema mchezaji huyo alishindwa kuafikiana na uongozi wa Yanga kufuatia mkataba mpya aliopewa.

Juma Abdul amekuwa ni nguzo muhimu kwa klabu ya Yanga eneo la ulinzi wa pembeni na msimu wa 2019/20 alicheza michezo 28 na alikuwa akifanya vyema. Msimu wa 2019/20 Abdul alifunga mabao 6 huku akitengeneza mengine 6 na kumfanya ahusike kwenye mabao 12 kati ya 45 yaliyofungwa na Yanga.

Mara baada ya kumalizana na Yanga Juma Abdul alinukuliwa akisema "umeshindwa kufikiana makubaliano na Yanga kwenye upande wa mkataba wangu kwa kuwa walitaka kunipa mkataba bila ya kunilipa fedha za usajili hivyo nimeamua kuanza maisha mengine," amesema.

Post a Comment

0 Comments