BETI NASI UTAJIRIKE

MZEE WA NANE NANE ALIVYOSAJILIWA NA AZAM MWEZI WA NANE


Unaweza kusema Ayoub Lyanga anabahati na  namba 8. Msimu wa 2019/20 mshambuliaji huyo alikuwa na mabao 8 huku pia akitengeneza pasi 8 za mabao kwenye klabu yake ya Coastal Union.

Mwezi huu wa  8 Azam FC kwa kutumia maskauti wamemnasa kiungo huyo  mshambuliaji na kumpa mkataba wa miaka miwili.Hivyo basi Lyanga atadumu na Azam mpaka mwaka 2023 kama asipouzwa.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wamekamilisha usajili kwa mapendekezo ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.

"Tumekamilisha usajili wa Lyanga kwa mkataba wa miaka miwili, bado kazi imeanza kwani huyu ni nyota wa tatu kwetu kutambulishwa.Hesabu zetu ni kuona kwama timu inakuwa imara zaidi na kuleta ushindani kwa msimu ujao, kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema.

Post a Comment

0 Comments