BETI NASI UTAJIRIKE

MWAKALEBELA AFUNGUKA MIPANGO YA YANGA NA MORISSON KUELEKEA MSIMU WA 2020/21
Inasemekana uongozi wa klabu ya Yanga unataka kumshughulikia haswa aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo Bernad Morrison.Taarifa za Uvumi zinasema Yanga wanajiandaa kumshtaki Bernard Morrison kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) pamoja na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili waweze kuamua suala la utata wao.

Utata wa mkataba wa Morrison na Yanga umezidi kushika kasi ambapo kila upande unavutia kwao.

Morrison anasema mkataba wake na Yanga ulikuwa ni miezi sita tu na tayari umeisha, huku Yanga wakisema kuwa ana mkataba hadi 2022.Nyota huyo alijizolea umaarufu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho wakati Yanga ikishinda mabao 2-0 mbele ya Prisons baada ya kutembea juu ya mpira.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alisema kuwa suala la Morrison uongozi umelichukulia kwa uzito jambo lililowafanya wapeleke mkataba wa mchezaji huyo CAF na FIFA.

“Tumepeleka mkataba wa Morrison CAF na FIFA, wao wana mamlaka kwenye masuala ya michezo, hatufanyi mambo kwa kubahatisha, hivyo hilo suala lake ninaweza kusema kuwa limekwisha.

"Mashabiki wasiwe na presha tupo sawa na tunajipanga kwa ajili ya msimu ujao mambo yakiwa sawa tutaweka wazi kila kitu," .

Post a Comment

0 Comments