BETI NASI UTAJIRIKE

MTAMBO WA MABAO NAMUNGO WATANGAZA KUITAKA YANGA


Habari za kuaminika zinasema mshambuliaji hatari wa Namungo raia wa Burundi Bigirima Blaise amegoma kusaini mkataba mpya a kuendelea kuitumikia timu hiyo.Taarifa za ndani zinsema mcheaji huyo ameshaanza mazungumzo na klabu ya Yanga .

mtu wa karibu na Blaise alisema, nyota huyo aliyemaliza ligi akiwa na mabao 10, amekuwa akimshinikiza meneja wake kufanya mpango wa kumtafutia nafasi ya kusajiliwa na Yanga, kwa kuwa ndoto zake kubwa ni kuona msimu ujao anavaa jezi ya timu hiyo.

 Habari za kuaminika kutoka ndani ya Namungo, zimeeleza: “Bigirimana amegoma kuongeza mkataba wa kubaki hapa Namungo kwa sababu tamaa yake kubwa ni kwenda kuichezea Yanga, amekuwa akisisitiza muda mrefu kuwa anatamani kuwa mchezaji wa timu kubwa kwa msimu ujao.”

 Bigirimana juu ya ishu hiyo amesema: “Kiukweli nataka kupata changamoto mpya msimu ujao, nimegoma kuongeza mkataba Namungo kwa sababu nataka kucheza timu nyingine. Masuala ya Yanga siwezi kusema, kama kweli yapo basi meneja wangu atakuja kuweka wazi.”

Post a Comment

0 Comments