BETI NASI UTAJIRIKE

MRITHI WA LUC EYMAEL APATIKANA NDANI YA YANGA


 Kocha Riedoh Berdien ndiye amekabidhiwa majukumu ya kukinoa kikosi hicho kilichoanza maandalizi ya msimu mpya wa 2020/2021.Kocha huyo ni kocha wa viungo wa timu hiyo na atainoa mpaka atakapopatikana kocha mkuu wa timu hiyo

Timu hiyo imeanza maandalizi yake Agosti 10,  kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria, Ubungo jijini Dar es Salaam kikiwa na kilianza na wachezaji 11 mwanzo kabla ya baadaye wengine kuongezeka.

Baadhi ya wachezaji wa mwanzo walioanza mazoezi ya timu hiyo wapya ni Yassin Mustapha na Waziri Junior hawa walikuwepo kwenye mazoezi ya siku ya kwanza wengine ni pamoja na Deus Kaseke ambaye amekabidhiwa kitambaa cha unahodha, Paul Godfery.

 Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli amesema kuwa timu hiyo itakuwa chini ya Bardien hadi itakapompata kocha mkuu.

Bumbuli amesema kuwa uongozi bado unaendelea na mchakato wake wa kumpata kocha mkuu kwa kupitia CV walizozituma kabla ya kufanya mchujo na kumpata mmoja bora atakayetangazwa hivi karibuni.

Timu hivi sasa ipo chini ya kocha msaidizi na viungo Berdien aliyebakishwa kwenye benchi la ufundi baada ya kuwaondoa baadhi ya viongozi akiwemo aliyekuwa kocha wetu mkuu Eymael.

“Hivyo kocha huyo ataendelea na majukumu yake hadi pale mchakato wa kumpata kocha mkuu utakapokamilika hivi karibuni baada ya kufanyika mchujo wa makocha 64 walioleta maombi yao ya kufundisha Yanga.

“Upo uwezekano mkubwa mchakato huo kukamilika ndani ya wiki mara baada ya kukamilika kwa taratibu zote, kikubwa tunahitaji kocha atakayekuwa bora,” alisema Bumbuli

Post a Comment

0 Comments